Mariah Carey |
Kumekuwepo
rumors zilizozagaa kwenye mitandao kuwa kuna beef la chini chini kati
ya Mariah Carey na Young Money rapper Nicki Minaj, ambao wote ni majaji
wa American Idol.
Rumors
hizi zilianza tu baada ya Nicki Minaj kutangazwa kujoin team ya majaji
wa AI, ambapo ilisemekana Mariah Carey hakupenda kabisa ujio wa Nicki
Minaj kama jaji wa AI na ikasemekana kuwa Mariah carry alipopigiwa simu
kuambiwa kuwa Nicki anajoin American Idol alikata simu baada ya
kusikia hiyo message.
The
R&B diva Mariah carry amefunguka kuhusu uvumi huu ili kuweka mambo
sawa kwa sababu ukimya wake ulizidisha kusambaa kwa rumors hizi.
Na ameonekana kutochukulia hizi rumors seriously, “How they could have sparked a feud in such a short time span?”
Mariah
aliuliza kwa shangao kwa sababu mashindano yenyewe yana siku mbili tu
na huu muda ndo unamfanya Mariah aulize mara mbilimbili inakuaje chuki
isambae hivi ndani ya siku mbili, “a feud takes a little longer to spread out, than that” alisema Mariah Carey huku akitabasamu.
Nick Minaj |
Katika
siku ya kwanza ya audition iliyofanyika New York City, MTV
iliwatembelea majaji hao ili kuona kilichokuwa kinaendelea na MTV
iliwashuhudia majaji hao wakitabasamu na kuwapokea vizuri tu, na
walipoulizwa kama ni kweli wanabeef wote walicheka na Mariah Carey
alimaliza kwa kusema “it’s fun, it’s music, it’s singing, it’s laughter.’’
Wakati huo Nicki yeye alitikisa kichwa na akaonekana anachekeshwa na hiyo rumors ya beef.
Hata
hivyo camera za MTV zilinasa jinsi ambavyo audition ilivyokuwa pale
New York City, na mara nyingi kullikuwa na mabishano kati ya Nicki
Minaj na Mariah Carey, wakati Nicki Minaj alipotoa comment zake kuhusu
alichofanya contestant, Mariah Carey aliingilia, na Nicki Minaj
alimjibu Mariah kwa sauti ya juu sana.
Ripoti
kutoka kwa Spy wa American Idol zinasema kuwa majaji hao wanajaribu tu
kuficha tofauti zao lakini kila mtu aliona wazi kabisa kupitia hiyo
audition ya kwanza pale NYC.
Haya
sasa siku mbili tu haya yote yamesikika, au kwa kuwa wote ni wasichana
wenye majina makubwa, hili zizi moja la AI litakalika hadi mwisho
watakapomaliza audition za Nchi nzima?