Wafanyakazi wa East Africa TV juzi walilazimika kutembea juu ya moto kama ishara kuwa wanaweza kukabaliana na changamoto zozote wanazokutana nazo mbele.
Zoezi hilo limefanyika baada ya kupewa semina ya siku mbili kutoka kwa wahamasishaji wa Peak Perfomance.
“Kutembea juu ya moto ilikuwa ni kuhamasisha moyo wa kujiamini na kuthubutu. Walilenga kumpa kila mtu morale ya kujitambua kuwa ana uwezo wa kufanya kitu unachohofia kuwa huenda huwezi kujichanganya,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa EATV.
Unaweza kutembea juu ya moto?