JUMA NATURE AWATAKA WASANII KUTOENDEKEZA NYIMBO ZA MAPENZI PEKEE...


Kama ulikuwa haujui Juma Nature yupo Facebook baada ya kuambiwa sana ajiunge na mtandao huo ili kuwa karibu na mashabiki wake. Kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo anatumia jina ‘Juma Natur Kibla’, msanii huyo mkongwe amewashauri wasanii wapya kutoendekeza nyimbo za mapenzi tu.

Nature ameandika, “Nawapa gwala madogo wote mlioingia kwenye game na mnafanya vizuri hadi sasa sema inabid mcibezi kwenye upande wa mapenzi peke yake coz kuna matatizo mengi sana yanayoizunguka nchi yetu na pia asanteni mashabiki wote mnaousapoti mzikii huu wa kibongo nawatakia kheri ya chrismac na mwaka mpya nawapenda wote.”