MSANII wa sinema na muziki wa Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,
Desemba 16, mwaka huu alinaswa gizani akiwa amejiweka kimahaba kwa mmoja
wa waimbaji wa mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), Antoine Christophe Agbepa Mumba ‘Koffi Olomide’,
Tukio
hilo lilitokea ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar,
ambapo Shilole alienda kwa ajili ya kushuhudia shoo ya mwanamuziki
huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja kama Shilole alimkubalia mshikaji huyo
lakini wadakuzi wanadai baada ya shoo kumalizika, mwanamuziki huyo
alimfuta tena Shilole na kuongozana naye hadi kwenye gari alilokwenda
nalo pale ukumbini.