Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.
Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na destruri ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.
Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho.