CHADEMA NA POLISI WAKUBALIANA KUSITISHA MAANDAMANO
CHADEMA
wamekubalina na Jeshi la Polisi Tanzania kusitisha maandamano
yaliyokuwa yafanyike kesho tarehe 25/03 kushinikiza kujiuzulu kwa
Mawaziri wa Elimu.
Upande wa CHADEMA kwenye mazungumzo hayo
umewakilishwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe na ule wa polisi
umewakilishwa na IGP Said Mwema. Pande mbili zimeafikiana kukutana tena
ndani ya siku 14 kwa ajili ya kuboresha mahusiano ya pande mbili.