Jumuiya ya waTanzania DMV yafungua Darasa la Kiswahili

Jumuiya ya waTanzania DMV imeweza kufanikisha darasa la kiswahili kwa watoto wao, jumla ya watoto (27) waliweza kuhudhuria katika darasa lililo funguliwa  rasmi siku ya Jumamosi, tarehe 23 March 2013  College Park Maryland Nchini Marekani.

Baadhi ya walimu waliojitolea kuwasomesha watoto akiwemo Mratibu wa darasa hilo na pia katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwana Amos Cherehani (Wakwanza kulia)  akitoa maelezo juu ya ufunguzi wa darasa la Kiswahili lililofunguliwa rasmi kwaajili ya watoto, Siku  ya Jumamosi, tarehe 23 March 2013  Callege Park Maryland Nchini Marekani. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)

Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa hilo waliweza kujiandikisha na pia kupangwa kwa makundi kutokana na uelewa wao wa kujua lugha ya Kiswahili na baada ya hapo watoto walijiandikisha na kuazishwa somu la kujua herufi za AEIOU.
Walimu walijitahidi sana kwa watoto waliojiandikisha na baadae kufundishwa kujua kuongea Kiswahili, chini ya Mratibu Mkuu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani na kumkaribisha Mgeni rasmi ambae alikua Rais wa Jumuiya ya waTanzania waishio DMV Bwana Iddi Sandaly.

Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwana Iddi Sandaly akiwakabidhi zawadi wanafunzi waliojiandikisha katika darasa hilo.
”Nimefurahishwa  sana na pia  nawashukuru sana wazee pamoja na walimu ambao wameshiriki kwa kujitolea pamoja na wazee kuwaleta watoto wao kwa lengo la kujifunza lugha yetu ya Kiswahili tuko pamoja na tutashirikiana kuendeleza utaratibu huu kwa watoto wetu”, alisema Bwana Iddi Sandaly,
Mpangilio mzima ulioazishwa wakukuza na kuitunza lugha ya kiswahili kwa watoto wa waTanzania wanaoishi DMV  ni kama ajira kwa watoto wetu alisema Mratibu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani ambae pia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV
Aidha Mratibu Mkuu wa darasa la kiswahili bwana Amos Cherehani aliwaomba waTanzania wanaoishi hapa DMV ambao wamebarikiwa kua na watoto wenye umri wa kwenda shule waje kujiunga na kuwaleta watoto wao kujifunza lugha ya Kiswahili bila ya malipo.

Baadhi ya watoto wanafunzi waliohudhuria kujiandikisha katika darasa la kiswahili na kuanza kujifunza kiswahili pamoja na kuhamasiswa wazee wajitahidi kuwafundisha kujua vitu tafauti kwa majina ya kiswahili.

Baada ya darasa walimu waliweza kuakabishi zawadi mbali mbali za kuweza kuwasaidi kujifunza kusoma na kuandika kiswahili zikiwemo madaftari pamoja na kalamu kwa kila mwanafunzi aliejiandikisha katika darasa hilo.

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Amos Cherehani pamoja na uongozi mzima akihamasisha watoto wanafunzi pamoja na wazee kuhusu umuhimu wa kuongea lugha ya Kiswahili Ughaibuni ni kama ajira alisema Mwenyekiti.
Video ya kuhamasisha