MSANII wa muziki na filamu Bongo, Saimon Mwapagata ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita.
Kwa
mujibu wa rafiki wa Rado ambaye pia ni msanii wa filamu, Deogratius
Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado alipokuwa akirudi
nyumbani kwake..
“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.
“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta mwizi wao.
“Nilipigiwa simu na msamaria na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa, kifuani na mguuni,”