Mashabiki
wa Bongo Flava wiki hii walisikitishwa na taarifa za Chidi Benz
kumpiga mshikaji wake Ngwair. Katika tukio hilo lililotokea Ambassador
Lounge jijini Dar es Salaam, Ngwair alidaiwa kujeruhiwa na chupa.
Tukio hilo lilimsikitisha pia mshkaji wao mwingine, Khalid Mohamed aka TID ambaye kwa mujibu wa U Heard ya Clouds FM, alipiga kioo cha gari yake kwa hasira.
“Hawa jamaa wanapigana pigana tu, me wananiudhi unajua kwanini , kwanini wao wanapigana pigana kila saa tu, huyu mara kampiga huyu and we all spend time together, at the end of the day wao wanaanza kupigana, mimi wananiconfuse, wananipotezea concentration ya kazi,” alisema TID.
“Hakuna sababu ya msingi watu wanapigana tu, watu wanongea saa zote tupo wote halafu baadae unaona watu wanaanza kupigana, unauliza sababu eti huyu kanambia mi dogo.. come on man. Mi nimewamind wote wanaopigana na ku disturb peace kwenye concentration ya kazi, violence inaonyesha sisi ni wajinga.”
Hata hivyo Chidi Benz aliendelea kusisitiza kuwa hakumpiga Ngwair. “Nani anaeamini Ngwea kapigwa? Y nimpige na ni mtu niko nae kila siiiku mabatani, tumefanya kazi nyiingi na tuna mipango,tafadhali usishabikie kitu na ukajiona mjinga mwishoni,” aliandika Chidi kwenye akaunti yake ya Facebook.
“Kuhusu swala la Ugomvi kati ya mimi na Mangwea naomba lisikuzwe ikaonekana ni sababu najua wabaya wangu watavyoweza kulikuza hili.hatuna Ubaya na ngwea na ni boonge la mshkaji..tusameheane haya Maisha tunatafuta.Peace, no lie.”