Ronaldo de Lima. |
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldo de Lima amesema kuwa hakuna ubishi kuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi kwasasa ndiye mchezaji bora wa dunia. Ronaldo mwenye umri wa miaka 35 amewahi kuicheza katika klabu ya Barcelona na Real Madrid ingawa anakiri pamoja na kuipenda zaidi Madrid lakini anampenda zaidi mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Argentina. Ronaldo pia aliipongeza Hispania kwa kunyakuwa taji la michuano ya Ulaya mwaka huu na kusifu kiwango cha kocha wa timu hiyo Vecente del Bosque kufanya vizuri kwenye michuano hiyo bila ya kuwa na mshambuliaji wa kutegemea. Nyota huyo amesema kuwa mchezo wa soka umebadilika katika kipindi hiki na anadhani Hispania walifanya kazi nzuri bila kuwa na mshambuliaji wa kutegemea kwani kwajinsi alivyomzoea kocha huyo wakati akifumfundisha alipokuwa Madrid alikuwa mara nyingi akimtumia kama mshambuliaji wa kutegemea katika kikosi hicho. Ronaldo alicheza Barcelona kati ya mwaka 1996 na 1997 baada ya kuitumikia Inter Milan ya Italia kwa miaka mitano na kurejea tena katika Ligi Kuu nchini Hispania na kutua katika klabu ya Madrid kabla ya kuondoka klabuni hapo mwaka 2007.