Kipigo
alichokipata Yanga katika mchezo wake wa awali dhidi ya Atletico ya
Burundi kimejirudia leo kwa watani wao wa jadi Simba ambao nao kama
Yanga wamechapwa goli 2-0 na URA ya Uganda.
Simba ilishuka katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo katika mchezo wake wa awali wa makundi kuwania kombe la Kagame.
Magoli la kwanza la URA lilipachikwa wavuni katika dakika ya 11 na mfungaji Feni Ali aliyevalia jezi namba 1O.
Wakati
Yanga jana ikifungwa goli la pili katika dakika za nyongeza ndivyo
ilivyokuta Simba leo baada ya kufungwa goli la pili katika dakika ya
90+2 kwa njia ya kichwa huku mfungaji akiwa yule Yule Feni Ali.
Magoli ya leo yote yamepachikwa kwa njia ya kichwa.
Wakati
huo huo Simba inaweza kujutia kumuacha mchezaji wake wa zamani Derick
Waluya ambaye leo alikuwa mlinzi mzuri na kizingiti kwa timu ya URA.
Mabingwa
wa Soka Tanzania bara na Urafiki, Simba ya Dar es Salaam hadi sasa ipo
nyuma kwa goli moja dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wa Makundi
Kombe la Kagame.