GUTI ATUNDIKA DALUGA.

Guti.
 KIUNGO nyota wa zamani wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Real Madrid, Jose Maria Gutierrez Hernandez aliyejulikana zaidi kama Guti ameamua kustaafu kucheza kucheza soka. Guti mwenye umri wa miaka 35 alikaririwa akisema kuwa kwasasa anatarajia kuchukua kozi ya ukocha aliyopewa na Madrid katika uwanja wa mazoezi Valdebebas. Mchezaji huyo ambaye amekuwa nje ya uwanja toka alipomaliza mkataba na Besiktas ya Uturuki Novemba mwaka jana, alishindwa kufikia makubaliano na kuhusu mkataba na klabu ya West Ham United ya Uingereza. Guti amekuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid kuanzia mwaka 1995 mpaka 2010 akiwa amecheza mchezo 387 na kufunga mabao 46 lakini alishindwa kuonyesha cheche zake katika kikosi cha nchi yake kwa kucheza mechi 14 pekee kati ya mwaka 1999 na 2005 bila kuchaguliwa katika michuano mikubwa.