WAKATI mademu kibao wa bongo muvi wakifanya michakato ya kufunga ndoa siku za usoni, Jackline Pantzel, maarufu kama ‘Jack wa Chuz’,
naye amedai kuwa kwa upande wake haoni kama ndoa hizo zinaweza kudumu
kwani wengi wanaona ufahari kutangaza kuwa wanafunga ndoa.
Kauli ya msanii huyo imekuja mara baada ya chanzo cha habari kuongea naye juu ya tabia walizonazo baadhi ya wasanii wanaopenda
kuweka hadharani mipango yao ya ndoa na mwisho wa siku hakuna
kinachofanyika.
Alidai kuwa wasanii wengi wanapenda kuzungumzwa na watu juu ya ishu hiyo lakini kikubwa wanachokifanya hakijulikani na wanapoulizwa hakuna majibu wanayotoa zaidi kidai kuwa vikao bado vinaendelea.
“Wapo wasanii wengi ambao nilisikia wanafunga ndoa lakini kadri siku zinavyozidi kwenda hakuna kipya, tena wengine utawaona kwenye kumbi za strarehe wanakula raha sasa mtu utajiuliza huyo si yupo kwenye mipango ya harusi na ni mchumba wa mtu inakuwaje anajiachia na huwezi kupata jibu,” alidai.
Aliongeza kuwa kwa hakika mtu anayehitaji kufunga ndoa kweli hawezi kujitangazia na hufanya mambo yake kwa umakini lakini, anawashangaa wasanii wa bongo muvi ambao kila kitu binafsi hupenda kukiweka hadharani.
Kauli ya Jack inawalenga baadhi ya wasanii ambao kila siku wanatangaza kuwa wanaolewa lakini siku na miaka inazidi kwenda na hakuna lolote.