MANCINI AKATA TAMAA NA VAN PERSIE.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amesema kuwa hategemei nahodha wa Arsenal Robin van Persie atajiunga na timu yake katika kipindi hiki cha usajili. Van Persie ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao tayari ameweka wazi Julai mwaka huu kuwa hatasaini mkataba mpya na klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa Emirates.
City, Manchester United na Juventus zimetajwa kumuwania mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi lakini Mancini akihojiwa hivo karibuni amesema kuwa hadhani kama mchezaji huyo atatua katika klabu yake. Van Persie ambaye ana umri wa miaka 29 amejumuishwa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kitakwenda Ujerumani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Uingereza hatahivyo haijajulikana kama atacheza katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Cologne utakaochezwa Jumapili.