Mavunde arejesha fomu za Umakamu Mwenyekiti UVCCM

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Antony Mavunde akirejesha fomu za kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma. Zoezi la urejeshaji fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za UVCCM ulitaraji kufikia tamati jana jioni kwa wagombea wote kutakiwa kutejesha fomu zao.
 
 Mavunde akionesha fomu yake kwa wanahabari kabla ya kuikabidhi.
 Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma akikagua fomu za Mazinde
 Mavunde akishuhudia ukaguzi wa fomu zake uliokuwa ukifanya na Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma
 Mmoja wa wagombea wa nafasi za ujumbe wa NEC akirejesha fomu
 Innocent Meleck nae alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti waliorejesha fomu za kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma.
 Daniel Zenda aki akirejesha fomu za kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa Mkuu wa Idara ya Siasa Oganizesheni ya UVCCM Taifa, Sophia Duma.
 Lulu Abas Mtemvu nae alirejesha fomu zake za kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM
Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mwanaamina Haji Mbarouk akipiga picha na Mgombea wa Nafasi ya Umakamu Mwenyekiti, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVVCCM Dodoma, Antony Mavunde.
Baadhi ya wagombea wakiwa katika mazungumzo baada ya kurejesha fomu zao katika Ofisi za UVCCM  Dar es Salaam.